Header Ads

Mwanaume mmoja amzika baba yake na gari ya thamani ya milioni miambili (200 milion) badala ya jeneza

Mwanaume mmoja anayejulikana kama Azubuike Raia wa Nigeria amewashangaza wengi baada ya taarifa zake kusambaa kwenye mtandao wa Facebook kwamba amemzika baba yake huku akitumia gari aina BMW kama jeneza.
 
Kwa mujibu wa duru za kuaminika zinasema kwamba gari hilo lina thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 200 za kitanzania ambalo limefukiwa chini kama jeneza ndani ya kaburi.

Aidha Mazishi hayo yalifanyika wikiendi iliyopita katika Mkoa wa Anambra nchini Nigeria ambapo ndipo yalipokuwa makazi ya baba wa Azubuike.
Powered by Blogger.